Makamu mwenyekiti wa TAVA, Muharame Mchume amesema wanatarajia kupata vipaji vipya katika michuano hiyo ambavyo vitazidi kuutangaza mchezo huu ndani na nje ya nchi.
Mchume amesema, mpaka sasa wana timu 10 shiriki lakini timu nyingine huongezeka mwishoni hivyo wanatarajia kuwa na timu zaidi ya 10 kutoka mikoa mbalimbali iliyo wanachama wa TAVA.
Mchume amesema, timu ya Makongo haina uhakika wa kushiriki michuano hiyo kutokana na kuwa katika michuano ya Shule za Sekondari Africa Mashariki lakini wanaamini ikiwahi kuwasili nchini itaweza kushiriki michuano hiyo na kuongeza idadi ya timu shiriki ambazo zitaleta ushindani katika michuano hiyo.
Mchume amesema, wanaamini watapata Klabu bora katika michuano hiyo ambayo itakuwa imefanya vizuri na itakayoendelea kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.


