
Nsajigwa amesema, vijana wanatakiwa kupata muda mwingi wa kucheza mpira na kuelekezwa sana ili kuweza kufikia mafanikio ya kuweza kuwa na vipaji vipya hapa nchini.
Nsajigwa amesema, ikipatikana nafasi ya kufundisha na vifaa vikiwa vya kutosha anaamini hakutakuwa na tatizo katika kukuza soka kwa vijana na haitachukua muda mrefu kwa vijana hao kuweza kufikia malengo katika soka.
Nsajigwa amesema, vijana wanatakiwa kupewa muda mwingi wa kucheza kwani wana vipaji vya asili hivyo vikiongezewa kidogo itakuwa rahisi kwa wao kuendelea katika soka.