Friday , 29th Mar , 2019

Tafsiri ya Uwanja wa Uhuru kuitwa 'Shamba la bibi' unaweza kuwa na sura mpya hivi sasa baada ya maboresho yanayoendelea kufanyika kuelekea michuano ya AFCON ya vijana wa U-17.

Muonekano wa Uwanja wa Uhuru

Uwanja huo uliitwa Shamba la bibi kutokana na timu nyingi kukimbilia kufanya mazoezi au kuchezea mechi, hali iliyopelekea hata kupoteza ubora wake wa eneo la kuchezea kutokana na kujaa mchanga na kuchakaa.

Hivi sasa uwanja huo uko katika matengenezo kwaajili ya Michuano ya Mataifa ya Afrika ya Vijana chini ya miaka 17, ambayo Tanzania itakuwa mwenyeji mapema mwezi ujao.

Nyasi za bandia zimeshaanza kutandikwa katika uwanja huo na kuufanya kuwa na muonekano wa kisasa kama viwanja vingine vizuri na vikubwa kama Old Trafford wa Manchester United na vingine vingi.

Sababu ya kubadili nyasi Uwanja wa Uhuru

 

Michuano hiyo ya vijana ya AFCON inazishirikisha nchi za Uganda, Senegal, Morocco, Angola, Cameroon, Guinea, Nigeria na wenyeji Tanzania. Jumla ya viwanja vitatu vitatumika, ambavyo ni Uwanja wa Uhuru, Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Azam Complex.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.