
Mayanja amesema, baada ya kumaliza mechi dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo pia waliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 alikipanga kikosi chake zaidi kwani anaamini hakuna timu nyepesi ambayo inashiriki Ligi kuu kwani kila timu inajipanga kwa ajili ya kuweza kuyibuka na Pointi tatu muhimu.
Katika taarifa yake Mayanja amesema, anaendelea kuwajenga wachezaji wake ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea katika msimu huu wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.
Mayanja amesema, anaamini kikosi cha Simba SC ni kizuri lakini anakifanyia marekebisho ili kuwa bora zaidi katika mechi zilizombele yao ambazo ni muhimu kwao kwa kuweza kuibuka na ushindi.