Friday , 11th Jul , 2014

Hatimaye mara baada ya kupatikana kwa uongozi mpya wa klabu ya Simba chini ya Rais wake Evans Aveva kuingia madarakani hivi karibu hii leo wamekabidhiwa rasmi ofisi na mali za klabu hiyo na uongozi uliopita chini ya mh. Ismail Aden Rage

Baadhi ya viongozi wapya wa klabu ya Simba ambao hii leo wamekabidhiwa rasmi ofisi na mali za klabu hiyo.

Uongozi mpya wa klabu ya soka ya Simba ya jijini Dar es salaam hii leo umekabidhiwa rasmi ofisi na mali za klabu hiyo kutoka kwa uongozi uliomaliza muda wake

Akikabidhi ofisi hiyo hii leo Rais mstaafu Ismail Aden rage amemtaka rais mpya wa klabu hiyo Evans Aveva kuhakikisha anarejesha umoja na mshikamano kwa kumaliza tofauti na wanachama walioshtaki klabu hiyo

Miongoni mwa nyaraka zilizokabidhiwa ni pamoja na hati za jengo la makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mtaa wa Msimbazi pamoja na kiwanja cha Bunju ambacho kimeanza kujengwa sehemu ya kufanyia mazoezi ya klabu hiyo pamoja na stakabadhi inayoonesha makubaliano ya malipo ya usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi ya Shirikisho la soka Duniani FIFA,kati ya timu ya Etoile du Sahel na klabu ya Simba fedha ambazo bado simba haijalipwa mpaka sasa

Pia Rage ameutaka uongozi wa Simba kuhakikisha wanaendelea kuitunza na kuithamini mikataba ambayo uongozi wake uliingia na makampuni tofauti kwa faida ya kalbu hiyo na wahakikishe wanapata wadhamini wengine wakiwemo pia wawekezaji hasa katika ujenzi wa kitega uchumi cha klabu hiyo katika makao makuu ya timu hiyo hapo msimbazi.

Naye Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amemshukuru Rage kwa mazuri aliyoifanyia klabu hiyo na ameahidi kuendeleza mazuri yote yaliyofanywa na uongozi uliopita na kikubwa ni kutekeleza ahadi ama ilani yao kama viongozi walioitoa wakati wakiomba kuchaguliwa kuiongoza klabu hiyo kwa miaka minne ijayo.