Mratibu wa umitashumta mkoa wa Morogoro Safari Nyerere amesema hayo wakati wa zoezi la uundaji wa timu ya mkoa inayotarajiwa kushiriki michuano ya umitashumta kitaifa jijini Mwanza.
Zoezi hilo limeambatana na kuchagua wanafunzi 80 watakaoshiriki michuano hiyo kwa nia ya kusaka vipaji ambapo amesema ukosefu wa vifaa na hali duni ya kifedha imefanya kusuasua kwa michuano hiyo, kwa kuwafanya washiriki kukosa usafiri na hata kupunguza morali ya wachezaji.
Akizungumza na wachezaji hao, afisa taaluma mkoa wa Morogoro Raphaeli mpangala amewasisitiza nidhamu ili kufikia malengo ya vipaji vyao, huku afisa michezo mkoa wa Morogoro Asteria Mwan'gombe akisema bidii kwa wachezaji hao itawapa umaarufu na kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa kitaifa na kimataifa..