Ikiwa imebakiza mechi 4 kufuzu michuano ya AFCON 2017 timu ya Taifa ya Uganda The Cranes inahitaji shilingi bilioni 1.8 kufanikisha mipango hiyo.
Rais wa shirikisho la soka nchini Uganda FUFA Moses Magogo amesema wanahitaji fedha hizo kiasi cha shilingi 1.8 kujiandaa na mchezo dhidi ya Burkinafaso, ili kufuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu 1978.
Magogo amesema wanahitaji ndege maalum ya serikali kuwapeleka Ouagadougou March 26, ili kuwahi kurudi kwenye mechi ya marudiano siku tatu baadaye mjini Kampala.
Serikali ya Uganda ilichangia kwa kiasi kikubwa maandalizi ya Cranes ilipoitoa Togo na kufuzu hatua ya makundi ya kombe la dunia 2018, nchini Urusi.
Kwenye mchezo huo uliofanyika mwezi Novemba mwaka uliopita, Rais Museven alitoa ndege, posho na kugharamia tiketi za ndege kwa wachezaji waliotoka nje ya Uganda kujiunga na kambi.






