Friday , 5th Jun , 2015

Uchaguzi wa chama cha mpira wa mikono uliotarajiwa kufanyika Agosti 15 umepelekwa mbele ambapo utafanyika Agosti 29 mwaka huu ili kutoa nafasi kwa wadau wa mpira huo kuchukua fomu.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa habari wa Baraza la michezo nchini BMT, Najaha Bakari amesema, wameamua kutoa nafasi kwa wadau wa mchezo huo ambao waliomba upelekwe mbele ili kupata nafasi za kuchukua fomu za uchaguzi huo kipindi cha likizo.

Najaha amesema, mpaka sasa wadau mbalimbali wameanza kuchukua fomu za uchaguzi huo ambapo anaamini mpaka mwisho wa kuchukua fomu ambapo ni Agosti 27 watakuwa wamefikia malengo wanayoyatarajia kwa ajili ya kukamilisha uchaguzi huo.