Friday , 27th Feb , 2015

Pambano la kuwania Ubingwa wa Afrika linatarajia kufanyika kesho kwa kuwakutanisha Mabondia Ibrahim Class na Cosmas Cheka.

Pambano la kuwania Ubingwa wa Afrika linatarajia kufanyika kesho kwa kuwakutanisha Mabondia Ibrahim Class na Cosmas Cheka huku Allybaba Ramdhan wa jijini Arusha akipanda kupambana na Jacob Maganga kutoka mkoani Tanga mapambano yatakayofanyika Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam, katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini PST Antony Rutta amesema licha ya pambano halo, kutakuwa na pambano la kumaliza Ubishi kati ya Francis Miyeyusho akikutana na Fadhili Majiha huku Ramadhan Shauri akipambana na Said Mungi.

Rutta amesema, pambano la Sadick Momba na Juma Mustapha litakuwa la mwisho katika mapambano hayo ya kumaliza ubishi huku mapambano ya utangulizi yakiwakutanisha wakinamama kati ya Lulu Kayange na Fatma Ally ambao watawania Ubingwa wa Taifa wa PST.