Thursday , 3rd Sep , 2015

Timu ya Taifa ya wanawake, Twiga Stars inayoondoka leo kuelekea nchini Congo Brazzaville kushiriki mashindano ya All Africa Games imesema inajihakikishia kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Kocha msaidizi wa Timu hiyo Edna Lema amesema, japo safari ilikuwa ikiahirishwa kila mara lakini kwa upande wao haijaathiri chochote kwani walikuwa wakiendelea na maandalizi ya michuano hiyo na wanaamini ushindi utapatikana kwa jitihada walizonazo.

Kocha Edna amesema, mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ivory Coast hapo Septemba sita wanaamini watafanya vizuri kwani kinachotakiwa ni ushirikiano baina ya wachezaji ili kuweza kufanya vizuri.