Tuesday , 31st May , 2016

Kikosi cha Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars kinatarajia kuingia kambini hivi karibuni kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Rwanda.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Alfredy Lucas, amesema timu ya Taifa ya Rwanda iliomba mchezo huo ikiwa ni katika maandalizi ya kusonga mbele katika kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wanawake.

Twiga Stars ilipoteza ndoto za kushiriki fainali za Afrika za wanawake mwaka huu baada ya kuchapwa jumla ya mabao 3-2 na timu ya Taifa ya wanawake ya Zambia.