Monday , 9th Nov , 2015

Kikosi cha JKT Ruvu kinachoshiriki michuano ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara kimesema, hakitakuwa na mapumziko kwa wachezaji wake ili kuweza kurekebisha mapungufu yaliyokuwa yakitokea katika mechi mbalimbali walizocheza.

Kocha msaidizi wa JKT Ruvu Mrage Kabange amesema, watasajili kwa ajili ya kuweza kufanya marekebisho madogo katika kikosi hicho ili kiweze kuwa kikosi bora zaidi katika mechi zinazofuata.

Kabange amesema, matokeo katika mechi zilizopita ni sehemu ya mchezo lakini kubwa zaidi ni katika safu ya ushambuliaji ambayo timu nyingi zinasumbuliwa na tatizo hilo lakini wanajitahidi kupambana nalo ili kuhakikisha vijana wanasimama vizuri na kuweza kupata mafanikio katika mechi zilizosalia.