Monday , 14th Sep , 2015

Shirikisho la soka nchini TFF limesema linasubiri ripoti ya kamishna ili kujua masuala mbalimbali juu ya viwanja na mtukio ya uwanjani katika michuano ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Celestine amesema, katika ufunguzi wa michuano hiyo katika mechi zilizochezwa Jumamosi na Jumapili kiujumla waliona kila kitu kilikuwa kama walivyopanga.

Mwesigwa amesema, ripoti itasaidia kuweza kujua mambo yaliyokuwa yakitokea ambayo kwa upande wao hawakuyaona hivyo kwa masaa 48 wanaamini watapata ripoti na kupitia kwa ajili ya kujua muenendo wa ligi hiyo.