Sunday , 25th May , 2014

Rais wa Oganaization ya ngumi za kulipwa nchini TPBO awatahadharisha mabondia wa hapa nyumbani kujipanga kwani TPBO itawaleta mabondia bora na wenye viwango vya hali ya juu na kama hawatajipanga wataishia kupoteza mapambano yao.

Rais wa TPBO Yasi Abdalah 'ustaadhi' katikati akiwa na mabondia wa kulipwa.

Mabondia wa ngumi za kulipwa nchini hivi karibuni wanataraji kupata mwokozi wao mara baada ya oganaization ya ngumi za kulipwa nchini TPBO kuwa katika hatua za mwisho kusaini mkataba ambao utawawezesha kuandaa mapambano sita ya kimataifa kila mwaka

Rais wa TPBO Yasin Abdalah Ustadh amesema mpango huo utawanufaisha sana mabondia wanaojitambua na amewataka mabondia wote kujipanga kutumia fulsa hiyo kwani ni mpango ambao programu yake itakua endelevu kwa kila mwaka

Ambapo kampuni hiyo ambayo hakutaka kuitaja amesema ndio itakua ikileta mabondia bora toka nje ya nchi ambapo kwa mwaka kutakua na mapambano 6 ya kimataifa yakihusisha mabondia toka nje ya nchi wakivaana na mabondia wa hapa nyumbani

Aidha Ustadhi amesema muda wowote kuanzia sasa pindi mabo yatakapokamilika basi watasaini mkataba na kampuni hiyo ambayo inamilikiwa na mmoja wa mapromota waliowahi kuandaa mapambano mengi ya kulipwa enzi za kina Rashid Matumla na baada ya hapo ndio atatangaza rasmi mbele ya waandishi wa habari.