Monday , 27th Jun , 2016

Kikosi cha TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kimewasili jana usiku tayari kwa mchezao dhidi ya Yanga hapo kesho Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji Mtanzania anayecheza TP Mazembe, Thomas Ulimwengu.

Mara baada ya kuwasili, mshambuliaji Mtanzania anayecheza katika klabu hiyo Thomas Ulimwengu ambaye kuda mwingi alikuwa akionyesha ishara ya vidole vitatu amesema, wanajua wamekuja kucheza na timu bora na wanaiheshimu Yanga lakini watapambana ili kuweza kushinda katika mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kwenda fainali.

Ulimwengu amesema, anaifahamu Yanga na wachezaji wake wengi ambao yupo nao timu ya taifa ya Tanzania na anaamini mchezo utakuwa mgumu.

Mabingwa hao mara tano wa Afrika watamenyana na Yanga katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika Jumanne katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mazembe imekuja na kikosi cha wachezaji 18 ambao ni; Robert Kidiaba, Sylvain Gbohou, Issama Mpeko, Joel Kimwaki, Thomas Ulimwengu, Christian Koume,
Jean Kasusula, Salif Coullbaly, Merveille Bope,Jose Badibake, Kissi Boateng, Roger Assale, Rainford Kalaba, Deo Kanda, Adama Traore, Chriastian Luyindama, Nathan Sinkala na Joas Sakuwaha.

Maofisa wa benchi la Ufundi wanaokuja ni Theobald Binamungu, Mohamed Kamwanya,Dony Kabongo, Frederic Kitengie na Andre Ntime. Madaktari ni Hurbert Velud, Pamphile Mihayo, Mhudumu Richard Mubemb na Maofisa wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Heritier Yinduka, Arther Kikuni na Meshack Kayembe.