Friday , 1st Jul , 2016

Klabu ya Crystal Palace imekamilisha usajili wa winga Andres Townsend kutoka Newcastle United ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano.

Winga wa Crystal Palace akionyesha jezi yake mpya mara baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo.

Townsend mwenye umri wa miaka ishirini na nne anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha Allan Pardew ambaye anakiandaa kikosi chake kitakachopambana msimu ujao wa ligi kuu ya England.

Winga huyo aliifungia Newcastle mabao manne katika mechi kumi na tatu alizocheza tangu atue klabuni hapo mwezi Januari akitokea Totenham Hotspurs.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa usajili huo mwenyekiti wa Palace Steve Parish amesema wanajivunia kupata saini ya nyota huyo ambaye anaamini uwepo wake kutaboresha kikosi chao kitakachofanya vizuri kuelekea msimu ujao.

Muingereza huyo aliyesajiliwa kwa dau la pauni milioni kumi na tatu anatarajia kuwaongezea washambuliaji Wilfred Zaha na Yannick Bolasie ambao wamekuwa wakianza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.