
Timu ya taifa ya ngumi nchini Tanzania inayojiandaa kwa mapambano ya ngumi katika michuano ya Jumuiya ya Madola imeendelea kujinoa katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es Salaam tayari kabisa kwa michuano hiyo.
Michuano hiyo itafanyika mapema mwezi wa saba mwaka huu katika jiji la Glasgow nchini Scotland, ambapo kocha wa timu hiyo Hassan Mzonge amejigamba kurudi na medali kadhaa katika mashindano hayo.
Endapo itafanikiwa kunyakua medali timu hiyo italeta faraja kubwa kwa mashabiki wa ndondi na Tanzania kwa jumla kutokana na mara nyingi timu za Tanzania kurudi nyumbani bila medali katika mashindano ya kimataifa.