Katibu Mkuu Chama cha Baseball Tanzania (TABSA) Alpherio Nchimbi (kushoto) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya mashindano ya Kitaifa ya mchezo wa huo.
Akizungumza hii leo Katibu mkuu wa mchezo wa Baseball na Softball nchini Alfepherio Moris Nchimbi amesema mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kwenye shule ya sekondari ya Azania ambao ndio wenyeji kwenye michezo hiyo.
Timu zitakazoshiriki michuano hiyo ni kutoka mikoa ya Mbeya,Kilimanjaro,Ruvuma,Kisiwani Zanzibar,Mwanza pamoja na Dar es salaam.
katibu huyo amesema timu saba kati ya tisa ni zile ambazo zinaundwa na umoja wa mchezo kutoka shule za sekondari huku mbili ni Tigers na Giants ambazo ni muunganiko wa wachezaji wa mchezo huo kutoka wanafunzi wa elimu ya juu yaani vyuoni.
ameongeza kuwa Mashindano hayo yatatumiwa na wataalamu wa mchezo huo kuteua timu ya Taifa ya umri chini ya miaka 21 itakayoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kutafuta viwango vya dunia yatakayopigwa nchini Africa Kusini mwezi februari mwakani.