Wednesday , 23rd Apr , 2014

Bondia machachari hapa nchini ambaye hivi karibuni alitwaa ubingwa wa Afrika wa UBO baada ya kumpiga Japhet Kaseba, Thomas Mashali amepata ajali mbaya alipokuwa akitoka mazoezini.

Thomas Mashali akionesha majeraha yake.

Bondia machachari hapa nchini ambaye hivi karibuni alitwaa ubingwa wa Afrika wa UBO baada ya kumpiga Japhet Kaseba, Thomas Mashali amepata ajali mbaya alipokuwa akitoka mazoezini wakati akijiandaa na pambano lake dhidi ya Kalama Nyilawila kuwania ubingwa wa kimataifa wa UBO lililopangwa kufanyika siku ya kilele cha siku ya mfanyakazi duniani yaani mei Mosi.

Mashali amesema gari lake lilitumbukia mtaroni maeneo ya Kinondoni na uskani kumbana maeneo ya tumboni na kupoteza fahamu.

Ajali hiyo imesababisha pambano lake dhidi ya Kalama Nyilawila lisogezwe mbele mpaka Mei 24 lakini itategemea na maendeleo yake ya kiafya.