Thursday , 23rd Apr , 2015

Shirikisho la soka nchini TFF limetakiwa kuwa makini na kuzichukulia hatua timu zote shiriki za ligi kuu soka Tanzania Bara ambazo zinaharibu michezo mbalimbali kwa kukiuka sheria 17 za soka.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa habari wa timu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema, zipo baadhi ya timu zinajaribu kuwa salama katika msimamo wa ligi lakini wanatumia vibaya sheria hizo.

Bwire amesema, kuna timu hazina uwezo wa kushika nafasi zinazohitaji kuwepo lakini hazina uwezo na zinalazimisha kuwa katika nafasi nzuri suala linalopelekea kuvuruga sheria 17 za soka hivyo kupelekea kushusha sifa na heshima za ligi kuu soka Tanzania Bara.