Afisa habari msaidizi wa TFF Mario Cliford Ndimbo amesema, mpaka sasa kamati ya waamuzi haijafanya mabadiliko ya waamuzi watakaochezesha mchezo huo.
"Kunataarifa zimekuwa zikisambaa kwamba kamati ya waamuzi imefanya mabadiliko kwa upande wa waamuzi watakaochezesha mchezo wa kesho kitu ambacho si sahihi'', amesema.
Aidha Ndimbo amesisitiza kuwa mchezo huo utachezeshwa na waamuzi walewale ambao Jonesia Rukya akisaidiwa na Sudi Lila, Hellen Mduma na Mwamuzi wa akiba atakuwa Isihaka Mwalile.
Simba na Azam FC zinakutana kesho kwenye mchezo wa raundi ya 17 na mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

