
Vijana wa Copa Coca Cola wakipambana katika michuano iliyopita
Shirikisho la Soka Tanzania TFF limesema litazingatia swala la udanganyaji umri katika mashindano ya Copa Coca-cola chini ya umri wa miaka 15 ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 13 hadi 20.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hii leo Mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana kutoka TFF Ayubu Nyenzi amesema mwaka huu hawatokuwa na mzaha katika kufatilia vyeti vya kuzaliwa kwa watoto hao, na kuwataka viongozi wa timu kufika na wachezaji wenye umri sahihi.
Nyenzi amesema endapo timu itagunduliwa inawachezaji waliozidi umri na wakapunguzwa na kubaki chini ya idadi ya wachezaji 16 timu hiyo itaondolewa kwenye mashindano kwa mujibu wa kanuni.