Monday , 27th Apr , 2015

Shirikisho la soka nchini TFF limesema, kozi mbalimbali za makocha zinasaidia kutekeleza mipango ya maendeleo ya mpira wa miguu katika nchi mbalimbali duniani.

Akizungumza jijini Dar es salaam, mmoja wa washiriki wa kozi ya makocha na wakufunzi ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga amesema, kozi hiyo ni sehemu ya mkakati wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF wa kubadilisha mpira ambapo kila mwanachama wa FIFA anawajibika na Programu ya kuondokana na mpira wa kizamani na kuwa na mpira wa kisasa.

Tenga amesema, kwa hali iliyopo sasa nchini Tanzania katika soka, inatakiwa kuongeza nguvu kwani nchi nyingine ziko mbali zaidi katika soka.