
Akizungumza na East Africa Radio Katibu Mkuu wa TBF Saleh Zonga amesema, wapo vijana wengi ambao wanafanyiwa mchakato wa kuweza kwenda kucheza nchini Marekani ambao wanauwezo na vigezo vya kuweza kujitangaza zaidi n akufika mbali katika mchezo huo.
Zonga amesema, Kocha kutoka nchini Marekani Mathew Mackolister anakuja Aprili mwaka huu nchini akiwa na lengo la kufundisha mchezo huu hapa nchini lakini pia anakuja na mfumo wa kukuza vipaji vingi ambavyo ataviona na pia ametoa vigezo vya vijana wanaotakiwa kwenda nchini marekani kwa ajili ya kuendeleza vipaji vyao.
Zonga amesema, wanaamini zoezi lao litafanikiwa kwani mpaka sasa wanavijana wengi ambao wanauwezo na wanandoto za kucheza nje ya nchi kwani sasa hivi michezo ni ajira hivyo kila mchezaji anatumia kipaji chake kama kazi.