Wednesday , 2nd Jul , 2014

Chama cha mpira wa wavu nchini Tanzania (TAVA) kimewataka wadau wa michezo hapa nchini kujitokeza kusaidia kwa kuudhamini mchezo huo ili kuutangaza na kufanya utambulike katika ngazi ya kimataifa.

Wachezaji wawavu wakifanya Mazoezi

Chama cha mpira wa wavu nchini Tanzania (TAVA) kimewataka wadau wa michezo hapa nchini kujitokeza kusaidia kwa kuudhamini mchezo huo ili kuutangaza na kufanya utambulike katika ngazi ya kimataifa.

Akizungumza na Muhtasari wa Michezo wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya walimu wa mchezo huo kutoka shule za msingi, Sekondari na Vyuo vikuu hapa nchini, Katibu mkuu wa Chama cha Wavu Nchini (TAVA) Alen Alex amesema timu nyingi zinashindwa kufanya vizuri katika mashindano mbali mbali yakiwemo ya kimataifa kutokana na kukosa maandalizi ya kutosha, ufadhili pamoja na vifaa.

Alex amesema mafunzo hayo yameudhuriwa na walimu wa mchezo huo kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa na lengo la kuukuza mchezo huu kwa kuanzia kwa vijana lakini kama wadhamini hawatajitokeza haitasaidia kukuza vipaji hivyo.

Tags: