Monday , 13th Apr , 2015

Chama cha Mpira wa wavu nchini TAVA kimesema wanaamini mafunzo kwa walimu kwa ajili ya mchezo huo ni msingi wa kuweza kupata wachezaji bora hapo baadae.

Akizungumza na East Afrika Radio, Makamu Mwenyekiti wa TAVA, Muharame Mchume amesema, kozi ya Cheti cha Daraja la kwanza wanayoipata walimu wa shule za msingi na Sekondari pamoja na makocha wa vilabu mbalimbali nchini inayotolewa na Level 1 katika mpira wa wavu, inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Wavu Duniani FIVB yataweza kuibua vipaji vitakavyoweza kuipeperusha bendera ya nchi.

Mchume amesema, walimu hao wapatao 30 wanaopata mafunzo kutoka kwa mkufunzi Kurt Radde aliyetokea nchini Ujerumani wataweza kusaidia kuweza kupata vipaji vipya vya mchezo huo ambavyo vitakuwa msaada mkubwa katika mashindano ya mashuleni.