Thursday , 6th Mar , 2014

Baada ya kushindwa mwaka jana kufanya sherehe za Tuzo kwa wanamichezo bora wa mwaka

Uongozi wa chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania TASWA umesema kuwa safari hii umejipanga vema kuhakikisha tuzo za mwanamichezo bora zinarejeshwa kwa kishindo, baada ya kukosekana mwaka jana kutokana na ukata,

Na katika kuhakikisha hilo linafanyika mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto amesema kuwa tayari wameshafanya mazungumzo ya kupata wadhamini watakaodhamini wa tukio hilo kubwa la kuenzi mchango wa wanamichezo mbalimbali hapa nchini

Pinto amesema kuwa mwaka jana walishindwa kufanya sherehe za utoaji tuzo hizo kutokana na kuwepo kwa kiasi cha shilingi milioni 30 wakati bajeti ya shughuli nzima iliitaji zaidi ya shilingi milioni 180.