Friday , 6th Jun , 2014

Matokeo mazuri dhidi ya The Mighty Warriors ya Zimbabwe yameibeba Taifa Stars kwa nafasi tisa duniani kutoka nafasi ya 122 mpaka ya 113 na pia nafasi tano kwa Afrika kutoka 37 mpaka 32.

Kikosi cha Taifa Stars kilichoitoa Zimbabwe kuelekea AFCON 2015 Morocco.

Shirikisho la soka la kimataifa FIFA, limetoa viwango vipya vya soka vya mataifa wanachama wake kwa mwezi wa sita.

Katika viwango hivyo, Tanzania imepanda nafasi tisa juu kutoka nafasi ya 122 duniani mwezi uliopita ilipokuwa na jumla ya points 226.70 mpaka nafasi ya 113 sasa ikiwa na jumla ya points 283.17. Pia imepanda nafasi tano Afrika kutoka nafasi ya 37 mpaka mwezi ulipita mpaka nafasi ya 32 mwezi huu.

Kupanda kwa Tanzania kunatokana na ushindi dhidi ya Zimbabwe katika mechi ya kuwania kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika litakalofanyika nchini Moroko mwakani.

Kwa upande wa nchi za CECAFA, Uganda inaongoza licha ya kuporomoka nafasi mbili Afrika kutoka nafasi ya 18 mwezi uliopita mpaka nafasi ya 20 mwezi huu lakini imebaki nafasi yake ile ile ya 86 duniani kama mwezi uliopita.

Ethiopia ni ya pili kwa CECAFA huku ikiporomoka nafasi moja Afrika kutoka nafasi ya 27 mwezi uliopita mpaka nafasi ya 29 na pia ikiporomoka nafasi 6 kidunia kutoka nafasi ya 101 mwezi uliopita mpaka nafasi ya 107 mwezi huu.

Na Tanzania imepanda nafasi moja juu kwa CECAFA kutoka nafasi tano mwezi uliopita mpaka nafasi ya nne mwezi huu.
Kwa upande wa Afrika Algeria imepanda nafasi tatu juu kutoka nafasi ya tatu Afrika na ya 25 duniani mwezi uliopita mpaka ya kwanza Afrika na ya 22 duniani mwezi huu

Kwa upande wa Afrika, Algeria imepanda nafasi tatu juu kutoka nafasi ya tatu Afrika na ya 25 duniani mwezi uliopita mpaka ya kwanza Afrika na ya 22 duniani mwezi huu.

Ivory Coast imeshuka nafasi moja kutoka namba moja Afrika namba 21 duniani mpaka namba 2 Afrika na 23 huku Misri ikiwa imeporomoka nafasi moja Afrika kutoka ya pili mpaka ya tatu na nafasi 12 duniani kutoka ya 24 mpaka ya 36.