Sunday , 29th May , 2016

Timu ya Taifa yaTanzania ‘Taifa Stars’ imelazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji Kenya ‘Harambee Stars’ katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa jioni ya leo Uwanja wa Kasarani, Nairobi, Kenya.

Timu ya Taifa yaTanzania ‘Taifa Stars’ imelazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji Kenya ‘Harambee Stars’ katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa jioni ya leo Uwanja wa Kasarani, Nairobi, Kenya.

Taifa Stars iliyotumia kikosi cha pili, ilianza kupata bao dakika ya 32 kupitia kwa mshambuliaji wa Stand United, Elias Maguli aliyemalizia kwa kichwa krosi ya beki wa kulia Juma Abdul.

Kenya wakapata penalti ya utata baada ya Ayoub Timbe kuonekana kujiangusha wakati akidhibitiwa na kiungo Deus Kaseke na Kiungo wa Southamptona ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza Victor Wanyama akaenda kufunga dakika ya 38.