Wednesday , 6th May , 2015

Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Mikono TAHA unatarajiwa kufanyika Agosti 15 mwaka huu.

Akizungumza na East Africa Radio, afisa habari wa Baraza la Michezo Tanzania BMT, Najaha Bakari amesema, fomu kwa ajili ya viongozi watakaowania katika nafasi mbalimbali za uongozi zimeanza kutolewa hapo jana.

Najaha amesema, nafasi zitakazowaniwa katika uchaguzi huo zipo 10 huku kwa upande wa TAHA wakiweka nafasi mbalimbali za ugombea tofauti na za BMT ili kuweza kuboresha na kukuza vilabu mbalimbali vya mchezo huo hapa nchini.