Monday , 4th May , 2015

Chama cha mchezo wa kuogelea nchini TSA kimesema kimeandaa mashindano yatakayokuwa yakifanyika mara moja kwa kila mwezi yakihusisha wachezaji 23 waliochaguliwa katika michuano iliyowashirikisha waogeleaji wa zamani yaan Masters Swimming.

Akizungumza na East Africa Radio, Mkurugenzi wa ufundi wa TSA, Marcelino Ngaliyoma amesema mashindano hayo ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya Afrika ya Masters pamoja na mashindano ya Afrika na mashindano ya Mexico yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2017.

Ngaliyoma amesema, mashindano hayo yanajumuisha waogeleaji wenye umri tofauti kati ya 25 na 60 ambapo watakuwa wakikutana mara kwa mara ili kuweza kuboresha timu hiyo na kuweza kufanya vizuri katika mashindano makubwa.