Monday , 21st Dec , 2015

Chama cha ngumi za ridhaa mkoa wa Iringa umesema umedhamiria kuhamasisha mchezo wa ngumi nyanda za juu kusini mwa Tanzania ili kuibua vipaji vilivyojificha vitakavyoweza kuitangaza nchi kimataifa.

Mwenyekiti wa chama cha ngumi za ridhaa mkoa wa Iringa akikutana na wanahabari mkoani humo.

Akizungumza na East Africa Radio mara baada ya kumalizika kwa mashindano yaliyohusisha mabondia wa mkoani humo hapo jana mwenyekiti wa chama hicho Samweli Sumwa amesema wameshaanza kuchukua hatua ya kuhakikisha wanaandaa mashindano ya mara kwa mara mkoani Iringa yakiwahusisha mabondi kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Sumwa amesema wanaamini kwa kuwa na mashindano hayo yataamsha ari kwa mabondia wao kujifunza vitu kutoka kwa wenzao waliopiga hatua kwenye mchezo wa masumbwi.

Mabondia kwa upande wa wanaume Batman Batmen,Hussein Kalambwanda ,na wale wa kike Rashida Ngairo,Salome Michael walipanda ulingoni jana kwenye viwanja wa Ccm Mkoani Iringa katika mapambano ya kufunga mwaka.

Kiongozi huyo amesema kwa sasa anatoa wito kwa viongozi wa ngumi mikoa ya Mbeya,Ruvuma,Njombe na Rukwa kuungana kwa pamoja kuinua mchezo wa masumbwi ili wafanye vyema mwaka ujao kitaifa.