Wednesday , 8th Jun , 2016

Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Nigeria, Stephen Okechukwu Keshi, ambaye pia aliwahi kuwa beki wa timu hiyo ya taifa 'Super Eagles' amefariki dunia.

Marehemu Stephen Okechukwu Keshi

Keshi aliyekuwa na umri wa miaka 54 amefariki dunia leo alfajiri huko Benin, ambapo taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Ben Olaiya.

Pia Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Nigeria, Ademola Olajire, amesema Keshi amefariki dunia baada ya kukimbizwa hospitali akilalamika miguu kuuma.