
Mchezaji wa Ligi ya NBA, Stephen Curry.
Curry,28, amesema majeruhi aliyonayo ndani ya msimu huu, ndio sababu kubwa ya kujitoa kwenye timu ya kikapu ya Marekani hivyo anataka muda wa kupumzika ili ajiandae na msimu ujao.
Curry alifunga pointi 18, alfajiri ya jana na kuisaidia timu yake ya Golden State Warriors kuongoza kwa ushindi mara wa 2-0 kwenye mchezo wa fainali ya pili, kati ya saba ya ligi ya NBA dhidi ya Cleveland Cavaliers.