Thursday , 24th Jul , 2014

Shirikisho la soka nchini TFF limesema timu ya Taifa stars itakwenda Msumbiji siku moja kabla ya mchezo ili kuepusha hujuma na vituko vya nje ya uwanja mabavyo vitaweza kuwavuruga wachezaji wa timu hiyo kisaikolojia na kuwatoa kimchezo

Mshambuliaji Mcha Hamis wa taifa stars akienda kuokota mpira baada ya kuifungia stars bao la kusawazisha dhidi ya Msumbiji

Kikosi cha Taifa Stars kimeondoka jijini Dar es salaam hii leo (Julai 24 mwaka huu) kwenda Mbeya ambapo itapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Msumbiji.

Mechi hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco itafanyika wikiendi ya Agosti 3 mwaka huu nchini Msumbiji.

Taifa Stars itaondoka nchini Julai 31 mwaka huu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini ambapo itafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kutua Maputo kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto na itarejea nchini mara moja mara baada ya mchezo huo.