Saturday , 29th Aug , 2015

Kocha wa Timu ya Taifa, Taifa Stars Boniface Mkwasa amesema, hali ya hewa iliyopo nchini Uturuki walipoweka kambi kujiandaa na mechi ya kufuzu fainali za AFCON dhidi ya Nigeria ina makusudi ya kuweza kuwaweka wachezaji katika hali nzuri kimazoezi.

Akizungumza na East Africa Radio kutoka nchini Uturuki Mkwasa amesema, hali ya hewa ya Uturuki ni ya baridi hivyo inasaidia wachezaji kuweza kujitengeneza kiafya kwa ajili ya kuweza kufanya vizuri katika mechi hiyo hapo Septemba tano Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo wa jana wa kirafiki dhidi ya Libya, Stars ililala kwa bao 2-1 huku bao la kufutia machozi la Stars likiwekwa kimyani na John Bocco Adebayor