Nahodha wa timu ya Flying Dribblers, Geofrey Lea
Akizungumza Nahodha wa Flying Dribblers, Geofrey Lea amesema imekuwa kama 'suprise' kwao kukutana na timu ya Mchenga BBall Stars ambayo walikuwa wanaitamani kwa muda mrefu tokea michuano hiyo ilipoanza kwa madai wanaifahamu vizuri mapungufu yao japokuwa ina uwezo mzuri kimchezo.
"Tunamshukuru Mungu kufika hii hatua ya kuingia nusu fainali, hatuja bahatisha kwa maana 'game' zote tumefanya vizuri, tunajua tunakutana na timu ambayo inazungumzwa na kutazamwa sana na sisi tunakubali nafasi yetu kama timu haipewi nafasi. Tunaamini maandalizi yetu yatakwenda sawa na kuhakikisha tunaondoka na ushindi", amesema Lea.
Kikosi cha Flying Dribblers
Kwa upande mwingine, Flying Dribblers waliweza kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kuwachapa Osterbay kwa point 91- 81 mchezo uliyochezwa Jumamosi Julai mosi katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).