
Aidha, katika mchezo wa kesho zitafahamika ni timu gani zitakazoweza kufuzu kuingia katika dirisha la pili la mashindano hayo kwa kigezo cha kuangaliwa tofauti ya vikapu, 'Goal difference' baina ya timu zote zilizoweza kupata ushindi wiki iliyopita pamoja na za kesho.
Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano Sprite BBall Kings timu ya Ukonga Warriors ndiyo itakuwa ya kwanza kuingia uwanjani dhidi ya Mchenga Team, ikifuatiwa na mechi ya pili ambapo Heroes B watakutana na wanafunzi kutoka chuo cha Ardhi University, mechi ya tatu itakuwa ni Flying Dribblers dhidi ya UDSM huku mechi ya nne itakuwa Kigamboni Heroes dhidi ya St Lous Montfort na kuhitimishwa na DMI dhid ya Osterbay kwa siku ya kesho.