Friday , 11th Apr , 2014

Wanariadha  nyota  kutoka  maeneo  mbalimbali nchini  kesho  wanatarajiwa  kuchuana vikali  katika  mbio za kilomita 10, zinazofahamika kwa jina la  Sokoine  Marathoni  zinafanyika  wilayani monduli  mkoani  Arusha.

Mary Naali, Mwanariadha wa Tanzania

Wanariadha  nyota  kutoka  maeneo  mbalimbali nchini  kesho  wanatarajiwa  kuchuana vikali  katika  mbio za kilomita 10, zinazofahamika kwa jina la  Sokoine  Marathoni  zinafanyika  wilayani monduli  mkoani  Arusha.

Wakizungumza  na  EATV baadhi  ya  washiriki  wa  mbio  hizo  ambazo  ni  sehemu ya maadhimisho  ya  kumbukumbu  ya miaka  30  ya  kifo  cha aliyekuwa  waziri  mkuu wa Tanzania Hayati  Edward  Moringe  Sokoine,  baadhi ya washiriki wa mbio hizo akiwemo  mwanariadha  nyota  wa mbio  ndefu  Marry  Naali  wamesema  wamejiandaa  vyema.

Pia wamesema  kwamba kupitia  mbio  hizo  wana  matumaini makubwa  na kuanza  kuboreka  kwa mchezo  wa riadha nchini.

Akizungumzia  mbio hizo  ambazo  mgeni rasm  anatarajiwa  kuwa  Rais  Jakaya Kikwete,  mkuu  wa  mkoa  wa  Arusha  Magesa  Mulongo  amewaomba wadau  mbalimbali  na  wananchi kujitokeza  kwa  wingi  kushiriki  mbio  hizo.