
Kikosi cha Simba SC, kikiwa uwanjani.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara kupitia ukurasa wake wa kijamii ikiwa ni dakika chache mara baada ya kumalizika mchezo huo ambao Mbao FC wametoka kifua mbele kwa bao 1-0.
"Bodi ya Wakurugenzi, sekretarieti, benchi la ufundi na wachezaji wa klabu ya Simba, wanawaomba radhi wanachama na washabiki wetu kwa matokeo ya leo. Tumeumia sote na tunawaomba mjue hii ni mechi ya nne tu. Tutafanya maamuzi sahihi bila 'pressure' kwa maslahi makubwa ya timu na klabu, nawaomba mtulie katika kipindi hiki", ameandika Manara.
Hiki ni kipigo cha kwanza kwa Simba katika msimu huu na kuendeleza mwenendo usioridhisha wa mechi za ugenini baada ya kutoka sare na Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara wikiendi iliyopita.
Matokeo hayo yanazidisha hofu kwa wanachama wa Simba kuelekea kwenye mechi ya watani wa jadi dhidi ya Yanga, inayotarajiwa kupigwa Septemba 30, 2018 huku kukitajwa kuwepo kwa mgogoro ndani ya klabu hiyo ikiwahusisha makocha.