Saturday , 17th Oct , 2015

Klabu ya Simba ya Dar es salaam, hii leo imevunja mwiko wa kushindwa kuifunga Mbeya City baada ya leo kuitungua katika dimba lake la nyumbani Sokoine jijini Mbeya.

Ilivyokuwa katika mchezo wa Yanga na Azam Uwanja wa Taifa

Klabu ya Simba ya Dar es salaam, hii leo imevunja mwiko wa kushindwa kuifunga Mbeya City baada ya leo kuitungua katika dimba lake la nyumbani Sokoine jijini Mbeya.

Bao la Simba limepatikana dakika ya 2 kupitia kwa beki wake Juuko Murshid baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Mbeya City.

Licha ya ushindi huo Simba ilionekana kuelemewa dakika za mwisho lakini safu yake ya ulinzi ikiongozwa na mganda Juuko Murshid ilikuwa imara.

Huu ni ushindi wa kwanza wa Simba dhidi ya Mbeya City tangu klabu hiyo ya halmashauri ya jiji la Mbeya iingie ligi kuu.

Katika dimba la Taifa Dar es salaam Yanga na Azam zimetoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 huku Yanga wakikosa penati katika dakika ya 86.

Wafungaji katika mechi hii ni Donald Ngoma kwa upande Yanga dakika ya 45 na Kipre Tchetche dakika ya 81.

Matokeo ya mechi nyingine zilizopigwa leo ni kama ifuatavyo:-
Coastal 0-1 Mtibwa
Majimaji 1-0 A.Sports
Ndanda 0-0 Toto
Stand 3-0 Prisons