Saturday , 18th Jun , 2016

Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa kiungo mchezeshaji, Mohammed Ibrahim 'Rasta' kutoka klabu ya Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili.

Timu hiyo, hadi hivi sasa imesajili wachezaji wanne akiwemo Rasta, Muzamir Yassin pia kutoka Mtibwa Sugar, Jamal Mnyate na Emmanuel Semwanza wote wa Mwadui FC.

Moja ya makubaliano ya Rasta na Simba ni kulipwa Sh 250,000 kila Simba inaposhinda yeye akiwa kikosini lakini dau lake la usajili limefichwa kwa sababu maalum.

Licha ya kuwasajili nyota hao, Simba bado inaendelea kufanya mazungumzo ya usajili na wachezaji wengine akiwemo kiungo wa Mtibwa, Shiza Kichuya.