Monday , 5th Dec , 2016

Simba SC inatarajiwa kwenda kuweka kambi Morogoro wiki hii huku watani wao Yanga wakiwa wamepanga kwenda Pemba wakati wowote kuanzia leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara mzunguko wa lala salama.

 

Pamoja na hayo, kocha mpya wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amesema, anataka mchezo mmoja wa kirafiki haraka ili kuwajua vizuri wachezaji baada ya kurithi timu kutoka kwa Mholanzi, Hans van der Pluijm katika mwezi uliopita huku Pluijm sasa akiwa ni Mkurugenzi wa Ufundi.

Kwa upande wa Simba, kocha Mcameroon Joseph Marius Omog amesema, amependelea zaidi timu kuweka kambi Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea katika mzunguko wa lala salama ambao unakuwa na ushindani kwa kila timu.

Simba SC walimaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu wakiwa wanaongoza kwa pointi zao 35, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga.