Wednesday , 24th Jan , 2018

Shirikisho la Mpira wa miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi watakaochezesha michezo ya kwanza na ya marudiano ya timu za Yanga kwenye ligi ya mabingwa na Simba kwenye kombe la shirikisho.

Yanga itacheza na Saint Louis FC ya Seychelles Februari 10, 2018 uwanja wa Taifa na utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia na Kamishna ni Frans Vatileni Mbidi wa Namibia.

Mwamuzi wa kati atakuwa Belay Tadesse Asserese akisaidiwa na Tigle Gizaw Belachew, Kinfe Yilma Kinfe, Amanuel Heleselass Worku na Kamishna Frans Vatileni Mbidi. 

Mechi ya pili itakayochezwa Seychelles kati ya Februari 20 na 21,2018 itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar, Andofetra Avombitana Rakotojaona akisaidiwa na Lionel Hasinjarasoa Andrianantenaina, Pierre Jean Eric Andrivoavonjy na Hamada el Moussa Nampiandraza.

Waamuzi kutoka Sudan Kusini Mwamuzi wa kati  Alier Michael James akisaidiwa na Abdallah Suleiman Gassim, Gasim Madir Dehiya na Kalisto Gumesi Simon Samson, wameteuliwa kuchezesha mechi ya kwanza kati ya Simba ya  na Gendarmerie Tnale ya Djobouti itakayochezwa Februari 21, 2018 Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa marudiano utakaochezwa Djibouti kati ya Februari 20 na 21, 2018 wenyewe utachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi Eric Manirakiza, Pascal Ndimunzigo, Willy Habimana na Pacifique Ndabihawenimana na kamishna ni Gaspard Kayijuka.