Friday , 11th Apr , 2014

Michuano ya Ligi Kuu ya soka ya Tanzania bara kuwania ubingwa inaendelea kesho katika raundi ya 25 ambapo Tanzania Prisons na Rhino Rangers zitaumana katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya.

Wachezaji wa ligi kuu Tanzania Bara wakichuana katika moja ya mechi.

Coastal Union itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es salaam,Afisa Habari wa Shirikisho la Kandanda nchini Tanzania TFF, wambura amesema Siku ya Jumapili ,Simba na Ashanti United zitapambana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Oljoro JKT na Mabingwa watetezi Dar es salaam Young Africans Maarufu kama Yanga.

Wambura amesema Mtibwa Sugar itacheza na Ruvu Shooting (Uwanja wa Manungu, Morogoro), Mgambo Shooting na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.