
Kocha Patrick Aussems na baadhi wa wachezaji wa Simba.
"Lazima tuhakikishe tunapata matokeo mazuri ugenini na nyumbani lakini katika mchezo huu ni lazima tubadilike kidogo kutokana na utofauti wa mchezo huu ukilinganisha na michezo ya ligi kuu maana JS Sauora tuliwafunga numbani nao watataka kutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani"- Denis Kitambi.
Simba inakwenda kucheza na JS Saoura kesho Jumamosi saa 4:00 usiku wakiwa katika nafasi ya pili na pointi 6 na endapo watashinda watafikisha pointi 9 huku wakisubiri matokeo ya AS Vita dhidi ya Al Ahly na kama mchezo huo utaisha kwa sare watakuwa wamefuzu robo fainali.
Mapema leo Simba wameondoka kwenye mji wa Algiers kwenda Béchar ambako ndipo utachezwa mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni mechi ya tano kundi D.