
Mlinda Mlango wa Yanga, Beno Kalolanya
Kakolanya amesema, Dida na Bartez ni makipa bora ambao anahitaji kujifunza mengi kutoka kwao na hajatua katika klabu hiyo kwa ajili ya kushindana nao bali ametua katika klabu hiyo kwa ajili ya imekuja kujifunza kutoka kwao.
Kakolanya amesema, wakati wote aliyokuwa Tanzania Prisons Dida na Barthez ndiyo walikuwa makipa chaguo lake na ameanza kujifunza kutoka kwao tangu anadakia Prisons na sasa amepata muda nzuri wa kuweza kukutana nao na kujifunza kwa karibu zaidi.
Kakolanya amesema nafasi ya kudaka Yanga itakuja kutokana na juhudi zake na wepesi wa kushika mafundisho ya mwalimu wa makipa, Juma Pondamali.