
Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa habari wa Shirikisho la Soka Nchini TFF, Baraka Kizuguto amesema, baada ya kuwasili kwa timu hiyo itafanya mazoezi yake ya mwisho Uwanja wa Karume.
Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Timu yua Twiga Stars, Rogasian Kaijage amesema, mchezo utakuwa ni mgumu lakini anaamini kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya kupata ushindi katika mechi hiyo.
Kaijage amesema, kutokana na ushindi wa mabao 4-2 walioupata katika mechi yao ya awali iliyopigwa nchini Zambia imekuwa ni changamoto kwa upande wao kuhakikisha wanapata ushindi katika Uwanja wa nyumbani.
Kaijage amesema, mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kikosi cha Zambia kujiandaa kwa ajili ya kupata ushindi lakini kitakachowasaidia ni ushindi walioupata hapo awali kuweza kuulinda ili kuweza kusonga mbele ingawa lolote kwenye soka linaweza kutokea.
Katika mchezo wa awali Twiga Stars ilishinda 4-2 hivyo kuhitaji sare au ushindi wa aina yoyote ili iweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya Afgrika kwa wanawake.