
Akizungumza na East Africa Radio, kocha Msabaha amesema vijana wanauelewa mkubwa katika mchezo huo suala linalopelekea kuwa na timu nyingi za watoto wanaoupenda na kuuelewa mchezo huo.
Msabaha amesema iwapo mchezo huo utaungwa mkono, utaweza kuliokoa taifa kwa kufanya vizuri katika mashindano makubwa ya ndani na nje ya nchi.