Wednesday , 9th Nov , 2016

Wizara wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeahidi kulisaidia Shirikisho la Soka nchini TFF katika kukuza na kuendeleza Ligi ya Wanawake hapa nchini.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema, soka la wanawake nchini linauwezo wa kufanya vizuri zaidi kama wakiwezeshwa na wao kama wizara yenye dhamana ya michezo nchini watahakikisha wanaisaidia TFF katika suala zima la kutafuta wadhamini kwani wanahitaji ligi hiyo ipanuke na kugusa maeneo mengi zaidi nchini.

Nape amesema, Ligi ipo katika hatua ya awali na anaamini kuwa wadhamini wengi hujitokeza Ligi inapochangamka, hivyo watajitahidi kuwashawishi ili waweze kuisaidia Ligi hiyo isiweze kupoteza mwelekeo wake katika ramani ya soka la wanawake.

Nape amesema, ni vizuri zaidi kusaidia ligi hiyo kwani waanzilishi tayari wana mfumo, muundo pamoja na morali ya kuendesha Ligi hiyo ambayo itatoa wachezaji wazuri zaidi wa Timu ya taifa ya wanawake